BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Hamasa ya mafanikio ya leo.

 


Iko wazi tu wakati wewe unalala, tambua wapo watu ambao hawalali, kazi yao ni kufanya kila mbinu na jitihada zote kuboresha maisha yao na yako pia.

Ndio maana kila siku unashangaa, mara kimegunduliwa hiki kipya mara kile, hayo ni matokeo ya kwamba watu hawalali, wanafanya kazi.

Na wewe leo amua kujipa zoezi, la kufanya kazi ili uboreshe maisha yako na ya wengine pia. Ukifanya kazi kila kitu kinawezekana kuwa safi.

Acha kila siku kuendelea kusema wachina ni noma, wachina ni wabunifu. Hao ni watu ambao wameamua kufanya kazi ili kuboresha maisha ya watu.

Kipi kinachokuzuia kufanya kazi. Amua leo kufanya kazi, na ukiwa siriaz, baada ya miaka mitano unakuwa sio wewe tena kimafanikio, utafika mbali sana.


Post a Comment

0 Comments