BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Hamasa ya mafanikio ya leo.

 

Kwa jinsi unavyoendelea kukifanya hicho unachokifanya, unayo nafasi ya kukifanya na kikawa bora zaidi.

Kwa jinsi unavyoendelea kuifanya kazi yako, hivyo ndivyo unaweza kuifanya kazi hiyo ikawa bora zaidi  na ya mafanikio.

Kwa jinsi unavyoendelea kuilea na kuitunza familia yako, pia hivyo ndivyo unavyoweza ukaipa furaha.

Kwa jinsi unavyoendelea kuishi, hivyo ndivyo unavyotakiwa uzidi kuwa bora na kufanya vizuri katika kila eneo la maisha yako.

Kwa chochote unachokifanya, ikiwa utaongeza juhudi kidogo kila siku, utafika mbali sana kimafanikio na hutaamini.

Kwa chochote unachokifanya, ikiwa utaamua kuuweka moyo wako hapo, na kukifanya kwa ubora wa juu, pia utafanikiwa.

Sio swala la muda, ni swala la mtazamo tu, kwa kila unachokifanya, unaweza kukifanya kikawa bora sana.

Amua leo, kuboresha maisha yako na yakawa mazuri zaidi, ikiwa kweli utaamua kufanya hivyo kwa jinsi siku zinavyokwenda.


Post a Comment

0 Comments