Ukweli na uhalisia wa mambo ambao upo wazi katika karne hii ya wasakatonge, zipo tafiti mbalimbali zenye kuhusu mahusiano ya kimapenzi ambazo zina na ukweli na nyingine ambazo hazina ukweli.
Miongoni mwa tafiti hizo zenye ukweli zinatabanisha ya kuwa wanaume wengi hawapendi kuombwa hela na watu walionao kwenye mahusiano yasiyo halali ( mahusiano yasiyo ya ndoa).
Sijui hata ni kwanini ipo hivyo, lakini pia hata ukijaribu kuwaauliza wanaume wengi ni kwanini hawapendi kuombwa hela au vitu vingine na wenzi wao wasiyo halali (walio nje ya ndoa), wanaume wengi huwa hawana majibu mnyooko yatakayosababisha akili yako iweze kuelewa ukweli uliojificha juu ya jambo hilo.
Hata hivyo ninalo jambo moja ambalo ni muhimu sana nataka kuongea viumbe hawa ambao tuliambiwa kuishi nao kwa akili kama ifuatavyo;
Kumuomba mwanaume vitu mbalimbali kama vile fedha, simu na mambo mengine kama hayo kwa upande wangu nadhani siyo dhambi wala siyo kosa ila ingefaa zaidi kwenu wakina dada kuwaomba wanaume vitu ambavyo wanaume hawa wana uwezo navyo.
Kwa mfano unakuta mdada anamuomba mwanaume amnunulie simu ya gharama kubwa wakati mwanaume huo hana uwezo huo, kitendo hiki kitakuwa ni kero kwa mwanaume huyo na kuona kuwa wakati mwingine wanawake ni wasumbufu sana linapokuja suala la kimahusiano hasa pale wanaomba vitu ambavyo wanaume hawana uwezo nayo.
Wanawake, ikiwa tunataka kufurahia mahusiano yetu ya kimapenzi ili tuweze kubalance mzani wa kimahusiano ambao husababisha wanaume wengi walalamike kuhusu suala la kuombwa vitu na wanawake, nadhani wanawake wangejifunza kuwaomba wanaume vitu ambavyo wana uwezo navyo na si vingievyo.
Muombe baiskeli mwenye uwezo wa kukunulia baiskeli, muombe simu ya kitochi mwenye uwezo wa kukunulia simu ya kitochi, muombe simu ya gharama mwenye uwezo wa kukununulia simu hiyo. Asante
0 Comments