Biashara nyingi zinazoanzishwa
haziwezi kufikisha miaka mitano, na hata zinazofikisha huwa hazina maendeleo
mazuri.
Hii ni kutokana na sababu biashara
nyingi huanzishwa kiholela, kienyeji, kimazoea, ukosefu wa mipango na mikakati
ya biashara. Pia, ukosefu wa utafiti wa masoko na kukosa utaalamu na ujuzi
mbalimbali katika biashara.
Katika kuanzisha biashara yako
unatakiwa kujifunza mbinu na ujuzi mbalimbali kadri unavyozidi kuifanya ili iweze
kufanikiwa. Kuna hatua ambazo ukizifuata biashara yako itafanikiwa.
Fanya
utafiti
Ukishakuwa na wazo la biashara
unayotaka kufanya, kinachofuata ni kuangalia uhalisia, jiulize je, wazo lako
lina uwezekano wa kufanikiwa? Unahitaji kuendeleza wazo lako huku ukiendelea
kufanya utafiti wa kina ili kupata uhalisia wa wazo lako kabla hujasonga mbele.
Ili biashara ndogo ifanikiwe lazima
ilenge kutatua tatizo, kukidhi mahitaji au itoe kitu ambacho soko linahitaji au
kuongeza thamani katika biashara husikKuna njia kadhaa zinazoweza kukusaidia
kutambua mahitaji hayo, hasa kufanya utafiti na kujaribu.
Kadri unavyotafiti soko, kuna
baadhi ya maswali ambayo lazima huyajibu; kuna uhitaji wa bidhaa/huduma yako?;
Nani anahitaji?; Kuna mtu au kampuni zinatoa bidhaa/huduma sawa?; Ushindani
ukoje? Na namna gani biashara yako itaingia sokoni?
Tengeneza
mpango wa biashara
Ili biashara yako iweze kufanikiwa
huna budi kuwa na mpango wa biashara wa namna ya kulifanyia kazi wazo lako.
Mpango wa biashara ni muongozo utakaokuongoza katika biashara yako kuanzia
hatua ya awali hadi inavyokua.
Mpango wa biashara unaweza kukupa
dira sahihi ya kile unachotegemea kufanikiwa katika biashara yako na namna gani
umepanga kufanya kitu hicho kiuhalisia, unaweza pia kutengeneza mpango kazi katika
daftari lako na ukaendelea kuboresha kadri mda unavyosonga mbele.
Pangilia
matumizi fedha
Kuanzisha biashara ndogo hakuhitaji
fedha nyingi sana, lakini itakuhitaji kufanya baadhi ya uwekezaji muhimu wa
mwanzo kama vile ufahamu wa biashara husika na uwezo wa kugharimia kadri
unavyoendelea kabla hujaanza kupata faida.
Weka pamoja daftari linaloonyesha
makadirio ya gharama ya kuanzisha na kuendeleza biashara yako kama vile vibali,
leseni, ada, ushuru, bima, vifaa, utafiti wa soko, matangazo, mshahara wa wewe
binafsi na wasaidizi wako, gharama ya pango, uzalishaji, gharama za
usafirishaji na usambazaji.
Chagua
mfumo wako wa uhasibu
Biashara ndogo zinaendeshwa vyema
na kwa mafanikio zaidi ikiwa kuna mifumo rasmi ya kifedha, mapato na matumizi
ikifanya kazi kwa weledi na kibunifu. Moja ya mifumo muhimu zaidi katika
biashara ndogo ni pamoja na mfumo imara wa uhasibu.
Mfumo wako wa uhasibu ni muhimu ili
kuunda na kuongoza bajeti yako, kupanga viwango na bei, kufanya biashara na
wengine pamoja na kodi.
Tengeneza
eneo la biashara
Kuandaa eneo lako la biashara ni
muhimu sana katika uendeshaji wa biashara yako iwe ni kwenye ofisi yako
nyumbani, ofisi binafsi ya biashara au eneo lolote biashara yako inafanyika.
Inakubidi ufikirie kwa kina kuhusu
eneo, vitendea kazi na mengineyo yote yanayohusika katika biashara yako,
hakikisha eneo la biashara yako linafaa kwa aina ya biashara utakayokuwa
unafanya.
Andaa
timu yako
Ikiwa utakuwa unaajiri watu
mbalimbali wa kukusaidia katika biashara yako, basi ni wajibu wako sasa kuanza
kutengeneza timu yako.
Hakikisha unapata muda wa kutosha
kuainisha nafasi, wajibu na sifa unazozihitaji katika kila kitengo cha biashara
yako. Utawala wa biashara ndogo una muongozo rahisi katika kuajiri watu kitu
ambacho ni muhimu kwa mwenye biashara ndogo kukua na kufanikiwa.
Tangaza
biashara yako
Ikiwa biashara yako tayari imeanza
huna budi kuanza kuvuta wateja katika huduma/bidhaa yako. Utahitajika kuanza na
mbinu na mikakati ya kimasoko na mauzo ya kipekee sana ili kuweza kufikia
wateja.
0 Comments