BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Mambo utayojifunza kutoka kwenye kitabu chaThe 5 AM Club (Own your morning, elevate your life) cha Robin Sharma

 



Kitabu cha "The 5 AM Club" cha Robin Sharma kina mafundisho mengi ya kusisimua! Hapa kuna mambo tisa ya kujifunza kutoka kwenye kitabu hicho:

1. Kuamka mapema. Kuanza siku saa kumi na moja asubuhi kunaweza kuleta mabadiliko makubwa katika maisha yako. Kwa sababu kunakusaidia kufanya mengi na yenye tija kabla hujaanza majukumu yaliyoko mbele yako.

2. Kupanga siku yako. Unapoamuka asubuhi na mapema kunakusaidia sana  kuweka malengo na mipango yako ya kila siku. Hapa ni lazima upange siku yako utakwenda kufanya nini, mambo haya ni lazima yawe ni ya mtiriko unaoeleweka. Ukiwa ni mtu mwenye ratiba inayoeleweka itakuwa ni rahisi zaidi kwako kupata mafanikio unayoyataka.

3. Kujifunza jambo jipya. Asubuhi akili yako inakuwa haina mambo mengi hivyo ndiyo muda wako wa kujifunza pia, hapa mwandishi anashauri kutenga muda kila siku kwa ajili ya kujifunza kupitia maarifa mapya yatakayokusaidia kupata mafaniko yako ambayo unayoyataka. Kila wakati jifunze vitu vitakavyokusaidia kuwa bora zaidi ya ulivyo leo.

4. Kuwekeza katika afya yako. Ukiamuaka asubuhi ni lazima utenge muda pia wa  kufanya mazoezi lakini pia kufanya mazoezi pekee haitoshi bali hakikisha unakula lishe bora ambayo itakusaidia kujali afya yako ya akili na mwili pia jambo hili ni muhimu sana kwa ustawi wako kijumla.

5. Gawa saa ya kwanza ya siku yako katika sehemu tatu. Dakika 20 kwa ajili ya  mazoezi ili uweze kuweka mwili wako katika afya njema. Dakika  20 zingine, hizi unatakiwa kuzitenga kwa ajili ya kujifunza ili uweze kuongeza maarifa na kuboresha ujuzi wako. Dakika 20 za mwisho ni kwa ajili ya kutafakari na kupanga kwa uwazi jinsi siku yako itakavyokuwa.

6. Kujenga mazoea mazuri. Unapoamka asubuhi unapaswa kujenga mazoea mazuri ambayo yatakufanya iwe ndiyo ratiba yako ya kila siku, mfano ratiba hiyo ni pamoja  na kusoma, kuandika na kutafakari yale yaliyo ya muhimu ambayo yatakusaidia kuweza kuwa bora kwa namna moja ama nyingine ambayo yatakusaidia kukupa mafanikio uyatakayo. 

7. Kuweka kipaumbele. Unapoaianza  siku yako usiianze kwa kukurupa pekee bali weka vitu kwa kufuata mpangilia wa utendeji wa kazi.  Kufanya kazi kwa vipaumbele kunaweza kuongeza ufanisi wako na kukusaidia kufikia malengo yako kwa ufanisi zaidi. Weka ratiba kwamba naanza hili kisha litafuta hili.

8. Kuwa na mshikamano. Mwandishi Robini anaeleze kuwa isipende kuwa mbinafsi, bali jifunze kufanya kazi kwa  kushikamana na watu wengine katika kufanya kazi, unapofanya kazi na watu wengine kunakusaidia sana kuweza kuvuka changamoto hatimaye kufikia mafanikio.

9. Kuwa na msingi thabiti. Mwandishi anasema lazima uwe na sheria binafsi zitakazokuongoza kufanya mambo yako. Kuweka misingi thabiti ya ufanyaji wa kazi kunakusaidia sana uwe ni mtu mwenye maadili ambapo kila jambo unalolifanya litasimamia maadili ya kazi zako na utaratibu uliyojipangia.

Hayo ni baadhi ya mambo muhimu yaliyoandikwa kwenye kitabu hiki, zaidi kitafute kitabu hiki ili uweze kusoma mwenyewe.

Tukutane tena kwenye uchambuzi ujao, siku ya jumapili saa tisa kamili hapa hapa mafanikio App.

Imeandikwa nami Benson Chonya

Post a Comment

0 Comments