BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Mambo muhimu ya kujifunza kutoka kwenye kitabu cha Think Again cha Adam Grant.

 


Kitabu "Think Again" cha Adam Grant kina mafunzo mengi mazuri! Hapa kuna mambo tisa ya kujifunza kutoka kwake:

1. Kuwa tayari kubadilisha mawazo. Mwandishi anasema kuwa mawazo yako pekee uliyonayo hayakutoshi kukupa mafanikio uyatakayo bali unatakiwa kuwa tayari kubapata mawazo mapya yatakayokujenga. Mawazo mapya utayapata kwenye kujifunza vitu vipya kila siku. Kila wakati kumbuka haukumbatii mawazo yako bila kuzingatia hoja mpya zitakazokupa ushahidi.

2. Kujifunza kutoka kwenye makosa yako. Jambo hili limesisitizwa na waandishi wengi wa vitabu, hata mwandishi  wa kitabu hiki cha think again bwana Adam ameandika pia huku akisema  Makosa ni fursa ya kujifunza na kuboresha mawazo yako. Hivyo unapokesea lipo la kujifunza hivyo usione aibu kokosea, kwani ukiona aibu unavyokosea ni wazi kwamba mafanikio yatajitenga nawe.

3. Kuuliza maswali mengi. Binadamu yeyote anayetaka kujenga dhana mpya yenye kuleta fikra chanya maishani mwake basi anapaswa kuwa na utaratibu wa kuuliza maswali.  Utamaduni wa kuuliza maswali husaidia  sana mtu kufikiria kwa kina na kuelewa mambo vizuri zaidi. Mawazo yako yatapanuka zaidi ukiwa na utaratibu wa kuuliza maswali.

4. Kusikiliza kwa makini. Uwezo pekee unatakiwa kuwa nao kwa sasa ni kusikiliza kwa makini.  Kusikiliza maoni na mitazamo tofauti kunaweza kukuza uelewa wako na kuongeza uwezo wako wa kufikiri. Jifunze kusikiliza vizuri ili uweze kuwa mjenga hoja mzuri pia. 

5. Kujua tofauti kati ya kile unachokijua na usichokijua. Mwandishi anasema kuwa na ufahamu wa kile unachojua na kile ambacho hujui kunaweza kukusaidia kuwa mwanafikra bora. Ambapo anasisitiza kwenye kile usichokijua basi tenga muda mwingi  wa kujifunza ili uweze kukijua na kile unachokijua basi haikisha hakisahau zaidi zaidi endelea kukifanyia kazi.

6. Kukubali kushindwa. Inapotea umeshindwa kwenye jambo fulani wala usijone ni mkosefu sana, elewa kushindwa kupo tu, pia elewa  kushindwa ni hatua muhimu  kujifunza na kukua kwako kama utaelewa vizuri katika kushindwa huko.  Unipotea umeshindwa tuliaza akili na anza upya pasipo kurudia makosa yale yale ya awali.

7. Kutafuta maoni ya wengine. Yapo mengi ya kujifunza hasa pale unapochukua maoni kutoka kwa watu wengine. Kupata maoni ya watu wengine kunaweza kukuza ufahamu wako na kukusaidia kufikiri kwa upana zaidi. Chukua maoni chanya yatakayokujenga pekee yale ambayo hayana mchango wowote ni vyema ukaachana nayo.

8. Kuwajibika na maamuzi yako. Mwenye kuwajibika na maisha yako ni wewe mwenyewe. Maamuzi yako sahihi ndiyo yatakayokutenga mbali na umaskini, hivyo unapaswa kuwajibika vyema na maamuzi yako kwa asilimia zote. Kuwa tayari kuchukua jukumu la maamuzi yako na kubadilika unapogundua kuwa unakosea hili litakusaidia sana kukupa kile unachokitaka.

9. Kuendelea kujifunza. Adam Grant anasisitiza suala la  kuwa na mtazamo wa kujifunza maisha yote na kukubali kwamba hakuna jambo litalokupa mabadiliko maishani kama hautakuwa mtu wa kujifunza, hivyo unapaswa kuwa mstari wa mbele kwenye kujifunza vitu chanya kwako. Jifunze kila jambo litalokuwa na tija kwako. 

Naamini kuna mambo umejifunza mambo ya muhimu zaidi kupitia maandishi haya.

Tukutane tena siku ya jumapili ijayo, muda ni saa tisa, hapa hapa mafanikio app.
Imeandikwa na Benson Chonya, afisa mipango.

Post a Comment

0 Comments