BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Mambo ya kujifunza kutoka kwenye kitabu cha The Magic Of Thinking Big cha David Schwartz.

 


Hapa kuna mafundisho 5 kutoka kitabu cha "The Magic of Thinking Big" kilichoandikwa na David Schwartz:

1. Amini nafsi yako na uwezo wako: Schwartz anasisitiza umuhimu wa kuamini nafsi yako na uwezo wako. Anahamasisha wasomaji kuendeleza mtazamo wa ujasiri na kujiamini, kwa kuondoa shaka na imani potofu. Ukiamini nafsi yako unakuwa una uwezo mkubwa wa kushinda hofu na vikwazo ambavyo vitakusaidia ili uweze kufanikiwa kwenye chochote ukitakacho. 

2. Weka malengo makubwa na chukua hatua kubwa: Schwartz anasisitiza suala la kuweka malengo makubwa ili uweze kupata mafanikio makubwa pia. Pia mwandishi anasema unapoweka malengo hayo thabiti kumbuka kuweka njia za kuweza kuyapata mafanikio hayo.  Usipange malengo makubwa pasipo kuweka njia pia ya kutimiza malengo hayo hapo utakuwa unacheza tu.

3. Weka mwenendo chanya wa akili: Schwartz anawafundisha wasomaji kuwa na mtazamo chanya wa kiakili kuhusu maisha ya mafanikio. Pia anasema mwenendo chanya wa akili ambao unapaswa kuwa nao ni pamoja na uwezo wa kipekee wa kubadili kila changamoto iliyo mbele yako kuwa fursa ya mafanikio. 

4. Chukua uwajibikaji kwenye maisha yako:  mafanikio makubwa huenda kwa mtu ambaye ni mwajibikaji mzuri kwenye maisha yake. Kwenye hili epuka kuwa mtu wa udhuru kila mara, unapaswa kufanya mambo muhimu, acha kuwa na visingizo visivyokuwa na maana. Unapokuwa mtu wa visingizio kumbuka unapoteza vingi sana.  Kumbuka kuwa mtu wa kuchukua hatua ili uweze kupata matokeo yaliyo bora kila mara.

5. Chagua marafiki walio chanya: Mwandishi anashauri kila wakati tujifunze kuwa na watu chanya kwa sababu watu chanya ni kichocheo kikubwa cha mafanikio. Tafuta marafiki ambao watakuhamasisha zaidi kuliko kuwa na marafiki ambao wao kazi yao kubwa ni kukukatisha tamaa kila wakati. Tafuta marafiki wenye mtazamo chanya, daima waepuke watu wenye mitizamo hasi hao hawakufai hata kidogo.

Kitabu the magic of thinking big kinauwezo mkubwa kwako ikiwa ni pamoja  na kufungua mitizamo mipya itakayokujenga, itaamsha ujasiri wa kufanya yaliyo makubwa pia kukutengenezea maisha unayoyatamani endapo yale uliyoyasoma utayaweka kwenye matendo.

Tukutane kwenye uchambuzi wa kitabu kijacho, siku ya jumapili.

Ndimi Afisa Mipango Benson Chonya

Post a Comment

0 Comments