BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Namna sahihi ya kuishi maisha yako ya kifedha bila majuto

Elimu ya hela na matumizi yake ni muhimu kuliko elimu nyingine yoyote kwa watu wanaofanya kazi za kuajiriwa na kujiajiri, jambo la kusikitisha ni kwamba haifundishwi mashuleni na ni asilimia  ndogo ya wazazi wanaofundisha watoto wao namna ya kutumia hela. Watu wanamaliza vyuo kikuu, wanaanza kazi na bado wanaishia kukopa na kushindwa kurejesha mikopo hiyo hii ni kwa sababu watu hao hawafahamu kiundani somo lianalohusu nidhamu ya fedha.

Pesa, pesa, pesa, Watu wengi wanaishi maisha yasiyo na furaha kutokana na matumizi mabaya ya pesa. Unakuta mtu anafanya kazi lakini anaishi mshahara kwa mshahara, huo ni utumwa usio na mkoloni.

Hivyo kila wakati unakumbushwa kutenga bajeti ya pesa zako unazozipata kama ifuatavyo;

Asilimia 30
Asilimia thelathini hakikisha inaenda kwenye kulipia kodi ya nyumba. Kama wewe tayari una nyumba, unaweza ukaweka asilimia 30 kwenye uwekezaji  (investment).

Asilimia 10 
Asiliamia kumi ya kipato chako hakikisha inaenda kusaidia ndugu na wasiojiweza. Jinsi unavyotoa hela ndio jinsi zinavyoingia, hivi ndivyo dunia ilivyo. Pesa hii kwa wale waoijua vyema dini huita ni fungu la kumi.

Asimilia 10 
Asilimia kumi nyingine hakikisha inaenda kwenye katika kuweka akiba, akiba hii ni ile ambayo itakusaidia hasa pale utapokuwa umepatwa na matatizo.

Asilimia 40 
Asilia arobaini unatakiwa kuifanya  ya matumizi yako ikiwemo chakula, usafiri, mavazi n.k.

Asilimia 10 
inayobaki inaenda kwenye matumizi yasiyokuwa ya lazima.

Ukifuata hii formula, utajikuta muda wote una hela kwenye akiba kwa ajili ya emergency. Hamna haja ya kwenda kukopa, au kusubiri mwisho wa mwezi ili uende kutembea bagamoyo. Bagamoyo unaenda muda wowote kwani tayari umeshaweka fungu lake pembeni. Ukiishi kwa namna hii utakuwa kuendesha   maisha yako na hutakuwa na matumizi makubwa kuliko kipato chako. Na kwasababu unaweka asilimia 10 kusaidia watu, utajikuta hela zinakurudia kwa namna ambavyo huwezi kuelezea.

Post a Comment

0 Comments