BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Mambo Kumi (10) Unayopaswa Kuyazingatia Katika Safari Yako Ya Mafanikio.


Yapo mambo ya msingi ambayo kila msaka mafanikio ni lazima ayafahamu katika safari yake ya mafanikio, na mambo hayo ya msingi yatamfanya mtu huyo aweze kuishi katika misingi hiyo ya mafanikio.
Na mambo hayo ni:
  1. Njia ya kuelekea kwenye mafanikio na njia ya kushindwa katika kufikia mafanikio mara nyingi zinafanana, hivyo ni vyema kila wakati ukajifunza kuchagua njia sahihi ya kukupeleka kwenye mafanikio unayoyoyahitaji.
  2. Mara zote ikumbukwe ya kwamba fursa zote unazoziona na usiziona huwa hazitokei kama ajali bali hutengnezwa hivyo jifunze kutengeneza fursa ili uweze kufikia katika kilele cha mafanikio yako.
  3. Kutengeneza mafanikio pekee yake haitoshi, bali jifunze pia kujitengenezea thamani kubwa katika jamii ambayo inakuzunguka, Thamani hii ina manufaa sana kwako na jamii inayokuzunguka.
  4. Kama hautakuwa tayari kupoteza au kupata hasara katika jambo lolote unalolifanya sahau kabisa kuhusu mafanikio.
  5. Kila wakati naomba utambue ya kwamba mafanikio hujengwa na msingi wa kutoka katika mazoea uliyoyazoea.
  6. Mara zote achana na tabia ya kuzungumza sana kuhusu malengo yako, bali unatakiwa kuyaweka malengo hayo katika vitendo.
  7. Hakuna siri za mafanikio isipokuwa na maandalizi thabiti ya mafanikio hayo, kufanya kazi kwa bidii na kujifunza kutokana na makosa unayopitia.
  8. Kama kweli unataka mafanikio na ili ufikie mafanikio hayo tambua unatakiwa kutokuwa mtu wa visinginzio hivyo epuka visingizio kila wakati.
  9. Mafanikio sio ufunguo wa furaha bali furaha ndiyo ufunguo wa mafanikio, hivyo ili uweze kuitengeneza furaha hiyo unatakiwa kupenda hasa kile unachokifanya.
  10. Kushindwa katika jambo unalolifanya isiwe kigezo ya kwamba huwezi kufanikiwa, bali unaposhindwa kama jambo fulani ndiyo fursa pia mara zote kumbuka kuanguka mara nane ni fursa ya kuinuka mara tisa.
Mpaka kufikia hapo sina la ziada cha msingi ni kuyazingatia hayo ambayo nimekueleza siku ya leo. Nikutakie siku njema na mafanikio mema.
Na: Ofisa mipango Benson Chonya

Post a Comment

0 Comments