Miongoni mwa mambo ambayo
huwa yananishangaza mbele ya macho yangu na maskio yako ni pamoja na kuona na
kusiakia eti kwa sababu amabazo siyo za msingi au wakati mwingine ikiwa ni wivu
tu, wapo baadhi ya wanaume wengi huwa hawaruhusu wake zao kujishughulisha na
kazi yeyote ile ya kuingiza kipato na
kuwafanya wake zao hao kuwa ni wakina mama wa nyumbani.
Mimi binafsi huwa
nashindwa kuelewa kwa nini wapo wanaume wenye tabia kama hizo? Kwa sababu kama
ambavyo wahenga waliwahi kusema “hakuna aijuaye kesho” hivyo yawezekana
leo wewe mwanaume u mzima wa afya tele na wewe ndiyo kila kitu kwenye ndoa hiyo
kwa maana wewe ndiyo mtegemezi wa kiuchumi kwenye familia yako ya ndoa.
Sasa itakuwaje endapo
utaumwa ghafla na hautakuwa na uhakika wa kuitegemeza tena familia yako? Na ili
hali hapo awali hukurusu mkeo awe na
shughuli ya kufanya ambayo ikingekuwa ni chanzo cha kutoteteleka kiuchumi hasa
pale wewe ukiwa huna uwezo tena wa kufanya kazi?
Nadhani katika hili basi
kwa kila mwanaume kwa nafasi yake basi ajitafakari na aone ni kwa namna gani
ambapo kila mmoja wetu anapaswa kuliangalia hili kwa namna ya tofauti na kuona
ni kwa namna gani mke wake badala ya kuwa ni mama wa nyumbani basi amruhusumama
mkewe aweze kuwa shughuli ya kufanya ambayo itakuwa inaiingiza kipato badala ya
kukaa na kusubiri mume peke ake awe ndiyo chanzo pekee cha kipato katika
familia.
Wapo baadhi ya wanaume
wanashindwa kuwaruhusu wake zao kujihusisha na shughuri mbambali eti kwa sababu
wanaona wake zao watakuwa wahuni, Pia nikukumbushe ewe mwanaume ya kuwa
unaposema mkeo akijihusisha na shughuri fulani basi utakuwa ni mwanzo wa yeye
kuwa mhuni, kitu hicho siyo kweli kwa sababu uhuni ni tabia kama mkeo ni mhuni
basi hata akikaaa nyumbani ni lazima atafanya uhuni tu.
Naomba nirudie tena kwa
kusema ya kwamba hakuna aijuaye kesho hivyo nadhani itakuwa jambo la busara
sana ewe mwanaume kuweza kumruhusu mkeo ajihusishe na kufanya kazi na si kuwa
mama wa nyumbani.
Ndimi
Afisa Mipango; Benson Chonya
0747030303
0 Comments