Mara nyingi tunapokuwa
kwenye mahusiano yetu ya kimapenzi basi tunapaswa kuwa makini sna na kauli
ambazo tunazitoa kwa wenzi wetu kwani zina uwezo ukubwa sana wa kuyavunja
mahusiano hayo.
Kauli hizo mara nyingi
huwa zinaanzia kwenye matamshi yetu ambayo tunayosema na wakati mwingine mpaka kwenye
yale tunayochati na wenzi wetu.
Kwa mfano unaweza ukakuta
mtu yupo kwenye mahusiano, kwa kuwa mpenzi wake amemuudhi basi anadiliki
kumwambia mpenzi wake wewe huna akili kabisa, mambo yako kama mtoto mdogo,
kwanza nipo na wewe basi tu, au anamtukana matusi makubwa ambayo siwezi
kuyaandika hapa au wakati mwingine kumfananisha na wanyama kama mbwa, paka na
wanyama wengineo.
Matamshi kama haya kwa
yule ambaye anayatamka huwa anaona yupo sahihi ila linapokuja kwa upande wa
mtukwanaji ni kitu ambacho huwa kinapokelewa katika mtazamo ambao siyo chanya
na wakati mwingi humuathiri kisaikolojia mtukwanaji huyo.
Wakati mwingine
mtukwanaji huyo huwa anawaza mengi kwamba hivi mimi ni kweli ndivyo nilivyo?
Hivi thamani yangu kwa mtu huyu ipo wapi? Mwisho wa siku mtukwanaji huyo
anajenga visilani visivyokuwa na maana, ambavyo hupelekea mwisho wa siku
kuvunjika kwa mahusioano hayo.
Binafsi naelewa kuwa
chanzo cha matusi ya namna hiyo hutokana na hasira kutoka kwa mtu aliyeudhiwa na mpenzi
wake.
Hata hivyo haijalishi
umeumia kiasi gani bada ya kuudhiwa na mwenzi wako nadhani litakuwa ni jambo la
busara sana kutafuta namna sahihi ya kuongea na aliyekuudhi na si kumtukana na
kumtakia maneno yasiyofaa kwani yana athari sana katika mahusiano yenu.
Hivyo niweke nukta kwa sema “ukitaka kujenga mahusiano yako ya kimapenzi
yaliyo bora zaidi basi jitahidi sana kila wakati kumtamkia mwenza wako yale
yatakayomjenga na si yatakayosababisha kuvunjika kwa muhusiano yenu”
Ndimi
Afisa Mipango: Benson Chonya
0747-030303
0 Comments