Hakuna mtu ambaye anaweza kupata uhuru wa kifedha kwa nguvu zake mwenyewe. Unahitaji msaada wa watu wengine. Tafuta watu wenye vipaji na uwezo ambao wewe hauna. Watu hao ni muhimu kwako.
Unatakiwa kujenga timu ya watu utakaoshirikiana nao, watu wanaotamani uhuru wa kifedha kama wewe. Jenga uhusiano na watu watakaokusaidia. Kama huna watu hao, ngumu sana kwako kufanikiwa.
Uhusiano
unaweza ukakujenga au ukakubomoa. Ndio maana unatakiwa kuwa mwangalifu sana na
timu unayojenga. Hakikisha timu inakuwa timu kweli ya kukusaidia na
kukuhamasisha na kujua vipaji.
Wako
rafiki katika mafanikio ; Imani Ngwangwalu
Bonyeza
hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail
BONYEZA HAPA http://wa.me/255687449428 ili kuwasiliana na Imani Ngwangwalu
kupitia WhatsApp.
0 Comments