Tabia yako halisi utaijua wakati ambapo unapitia magumu kwenye maisha yako. Wakati unapitia mazuri, sio rahisi sana kujua tabia yako, zaidi unaweza ukawa unaigiza tu.
Utaijua tabia yako halisi pale ambapo mambo yanakuwa magumu, pale ambapo umekutana na changamoto kubwa, na pale ambapo unaona kila kitu hakiendi kabisa.
Wakati wa magumu ndiyo wakati unaoweza kupima imani yako binafsi, misimamo yako na vipaumbele vyako. Pia ndiyo wakati unaoweza kupima mahusiano yako na wengine.
Wakati mwingine tunapitia magumu kwenye maisha yetu, ili tuweze kujifunza kuhusu sisi wenyewe. Unapokuwa unapitia ugumu, usiishie tu kulalamika, jifunze tabia zako halisi.
Wako
rafiki katika mafanikio ; Imani Ngwangwalu
Bonyeza
hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail
BONYEZA HAPA http://wa.me/255687449428 ili kuwasiliana na Imani Ngwangwalu
kupitia WhatsApp.
0 Comments