Kuna vitu vingi tunahitaji kwenye maisha, lakini wengi hatuna mpango wa kuvipata. Unahitaji mpango ili kupata hivyo unavyohitaji kupata. Kama huna na mpango huwezi kuvipata.
Unahitaji mpango wa miezi 3, miezi 6, hata mpango wa mwaka mzima. John Beckley anasema ” watu hawapangi kushindwa, wanashindwa kupanga”. Hivyo, mpango ni muhimu sana kwako.
Usiwe na mawazo tu kichwani bila kuwa na mpango wa kuyatekeleza hayo mawazo. Kama unategemea kupata kitu fulani kwenye maisha, lazima uwe na mpango wa kukipata.
Kama unataka kuwa na uhuru wa kifedha, lazima uwe na mpango. Kama uko makini, lazima uwe na mpango. Watu wanaotegemea kufanikiwa, wana mpango. Je, una mpango wa mafanikio yako.
Vitu vyote vinavyokuzunguka kabla havijawa na muonekano unao uona leo, kulikuwa na mpango kwanza. Kuanzia nyumba yako, viti, gari na vingine vilianza kama mpango.
Hakuna
kinachojengwa bila mpango kuwako kwanza. Mpango ndio unaanza na baadae
kinajengwa. Lazima utengeneze mpango wa kule unakotaka kufika kabla ya kufika.
Wako
rafiki katika mafanikio ; Imani Ngwangwalu
Bonyeza
hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail
BONYEZA HAPA http://wa.me/255687449428 ili kuwasiliana na Imani Ngwangwalu
kupitia WhatsApp.
0 Comments