BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Hamasa ya mafanikio ya leo.

Kama leo hii ikitokea ulikuwa eneo la barabarani, na ukaulizwa magari mangapi ya rangi nyekundu umeyaona, itakuwa ngumu sana kwako kukumbuka, pengine hata moja unaweza ukawa hujaliona.

Hiyo iko hivyo kwa sababu, kile ambacho hujaamua kukitafuta, sio rahisi kukiona. Unakiona tu kile unachokitafuta. Ndio maana biblia inasema, "tafuteni nanyi mtapata, ombeni nanyi mtapewa." Huo ndio ukweli wa mambo.

Ni kipi ambacho kweli unakitafuta kwa moyo wako wote na ukakikosa? Je, unatafuta mtaji, pesa, gari au nyumba?  Amini, chochote utakachoamua kukitafuta utakipata, ikiwa utatumia nguvu na akili.

Leo hii, amua kutafuta maisha unayoyataka, na kwa sababu umeamua kweli kuyatafuta maisha hayo, utayapata kwa jinsi unavyotaka na hakuna mtu wa kuweza kukuzuia. UNAPATA KILE UNACHOKITAFUTA.


Post a Comment

0 Comments