BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Hamasa ya mafanikio ya leo.

Kuna wakati Dr. Robert Schuller, aliwahi kuuliza, utafanya kitu gani ikiwa utajua kitu hicho hata ukikifanya lazima ukipate au lazima ukifanikishe?

Kama leo hii wewe ungeulizwa swali hilo, naamini ungetaja vitu vingi sana, kwa nini, ni kwa sababu ungejua hata ukifanya huwezi kushindwa kwa hiyo ungejitajia tu ili ufanikiwe.

Watu wengi wasio na mafanikio, ndivyo walivyo, wanaogopa sana kushindwa, wakati watu wenye mafanikio wao hawana hicho kitu kinachoitwa kushindwa kwenye maisha yao kabisa.

Kama unaogopa kushindwa, unatakiwa ujikumbushe ya kwamba kuna MATOKEO. Ukiona umeshindwa, jifunze kwa waliofanikiwa kwa jambo hilo na wewe lifanye kwa mafanikio na utapata matokeo bora.

Kama wewe unaamini kushindwa kuna kushusha chini, basi unajipoteza na unajipotezea mwelekeo wako wa kufanikiwa na kuona mambo.

Jikumbushe, kila kitu unachofanya kina matokeo. Kama unapata matokeo ambayo huridhiki, yaani unashindwa mara kwa mara, waulize waliofanikiwa kwenye eneo hilo, watakupa siri ya mafanikio yao.

Hivyo, wewe usiogope kushindwa, kwani hayo ni matokeo yanayokuonyesha wewe hujui vitu fulani, chukua kama fundisho, badilika na utafanikiwa.


Post a Comment

0 Comments