Ni nani anayeongea na wewe muda mrefu kuliko mtu yeyote. Je, umeshawahi kujiuliza ni mtu yupi anaongea na wewe sana? Je, ni boss wako, mke wako, wafanyakazi wako au nani?
Kama umeshawahi kujiuliza hivyo, jibu lake ni jepesi tu, anayeongea sana na wewe, ni wewe mwenyewe. Ndani yako unayo sauti ambayo inaongea sana na wewe kuliko mtu yeyote yule.
Kila siku kupitia sauti ya ndani, unaongea sana na wewe kuliko mtu yeyote. Sauti hiyo ya ndani kuna wakati inakushauri fanya hili au usifanye hili au fanya hiki au kile, hiyo ni sauti ya ndani yako.
Jukumu lako ni kuibadilisha sauti ya ndani, inayokushauri kila wakati, na kuwa na mategemeo bora. Hakikisha sauti yako ya ndani inasema yale yaliyo bora tu na sio kinyume chake.
Ukiwa na sauti ya ndani bora, ukiwa unajisemea kwa ubora hata maisha yako pia yatafanikiwa. Ukiwa unajisemea vitu vya hovyo, utapata shida sana kufikia mafanikio yako.

0 Comments