Kuna wakati unaweza ukajikuta unatafuta wateja wapya lakini huwapati, unatafuta kuongeza mauzo lakini aah wapi hayaongezeki, unafikiria kila njia, lakini majibu unakuwa hupati.
Pia kuna wakati kuna changamoto au tatizo fulani linakusumbua sana, unawaza weee njia ya kukabiliana nalo hata huioni, unabaki unashangaa utafanya nini au utumie njia ipi ya kulikabali.
Lakini, pia unashangaa, unapoacha tatizo hilo kwa muda, kwa mfano hata huwazi jinsi ya kulitatua labda kwa siku mbili au tatu, unashangaa majibu yanapatikana kirahisi sana.
Kinachotokea ni kwamba, wewe unakuwa karibu sana na tatizo lako, ndio maana unakuwa hupati majibu sahihi. Ukikaa mbali kidogo na tatizo lako, utaliona kwa ufasaha tu na majibu utapata.
Hatua ya kuchukua, kama kuna tatizo linakusumbua na hulipatii majibu yake, usitafute njia ya moja kwa moja, liache kwa muda, halafu rudi kutafuta njia upya, majibu yake utayapata tu.

0 Comments