BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Hamasa ya mafanikio ya leo.

 Je, unataka kila unachosema uweze kusikilizwa kirahisi bila pingamizi? Kwa mfano, unataka usikilizwe na wanaokusikiliza au usikilizwe na wateja wako au jamii inayokuzunguka.

Kama iko hivyo ni rahisi tu, anza kuongeza neno kwa sababu, kwa chochote kile unachokisema, ukishamaliza kuongea wewe ongeza neno kwa sababu na uone matokeo yake.

Kwa mfano, naenda kuanza biashara hii, kwa sababu....

Naamini  ugonjwa huo utapona, kwa sababu...

Naamini tutavuka katika hili bila shida, kwa sababu...

Naamini Mungu atatusaidia kwa yote tunayopitia, kwa sababu...

Naamini wewe ni mshindi katika mafanikio yako, kwa sababu...

Naamini utashinda changamoto zote, kwa sababu...

Ukijifunza kuongeza kwa sababu kwenye maongezi yako utasikilizwa na kuaminiwa kwa kiasi kikubwa sana. Ongeza kwa sababu, utaona unafanikiwa kusikilizwa kwa kiasi kikubwa.


Post a Comment

0 Comments