Ikiwa imefika mahali na ukahisi unataka kukata tamaa, kwa sababu ya changamoto, basi tambua, ndoto zako hazijawa kubwa kivilee, wenye ndoto kubwa ni watu ambao hawakati tamaa.
Chochote unachokifanya, elewa kina changamoto, kwani hakuna kisicho na changamoto na changamoto hazipo kukuzuia kufanikiwa bali kukufanya ukue na kuwa mkomavu wa kujua kipi kinatakiwa na kipi hakitakiwi.
Kuwa na shukrani hata zinapotokea changamoto. Hakuna mtu ambae anaweza akapata mafanikio makubwa sana, kama hakutani na changamoto, hivyo, acha kulia unapokutana na changamoto chukulia kama fundisho.

0 Comments