Maarifa yaliyopo kwa sasa kila baada ya miaka 3 hadi 5 yanaongezeka mara mbili, na hata teknolojia nayo pia inabadilika na kukua kwa kasi sana, na mambo mengi yanaongezeka.
Njia sahihi ya wewe kujua mambo mengi yanayoongezeka kila siku ni kufanya, kujifunza kuwa zoezi endelevu na la kila siku. Kama ukijifunza kila siku, ongezeko la maarifa litakusaidia sana.
Watu wengi hawasomi mara baada ya kumaliza shule, huko ni kujitakia kushindwa kuliko, tunasema ni watu ambao wanakuwa wanatafuta 'Recipe for failure' yaani wanajitafutia tiketi ya kushindwa.
Kila kitu ulichonacho, baada ya muda kitapotea au kitakuwa hakifanyi kazi vizuri kama hutajifunza. Wekeza nguvu zako katika kujifunza na utaona mabadiliko ya maisha yako kama utaboresha mambo ya msingi kila ukijifunza.

0 Comments