Maisha ya mafanikio, hayatafsiriwi, kwa wewe kuwa na vitu vingi, bali yanatafsiriwa kwa wewe jinsi unavyoboresha maisha yako. Hivyo, ndiyo maisha ya mafanikio yanavyotafsiriwa na sio vingine.
Kama una vitu vingi, mfano mali za kutosha na halafu maisha yako yakawa hovyo. Vitu hivyo bado havikusaidii, kwa sababu bado haviboreshi maisha yako na bado uko hovyo.
Inaeleweka wazi tu, wewe huna muda wa kufanya kila kitu, fanya mambo machache na kwa ubora. Acha kutanga tanga, na mambo mengi, tulia na mambo machache yanayoboresha maisha yako.
Kama ukijihusisha na mambo machache, na mambo hayo ukayaona yamekupa faida, basi utafanikiwa na kufika mbali kimafanikio zaidi na zaidi tena, kama utayakazania kisawa sawa mambo hayo.

0 Comments