Ipo siku utaangalia nyuma ya maisha yako utajishangaa, ni kwa nini hukuchukua hata hatua mapema na ukabaki unashangaa shangaa tu bila sababu ambayo ulikuwanayo na ukabaki hivyo?
Ipo siku utaangalia nyuma ya maisha yako na utashangaa ni kwa nini uliruhusu mambo madogo madogo, yakushushe chini na kukupotezea mwelekeo wa mafanikio yako.
Ipo siku utaangalia nyuma ya mafanikio yako na utashangaa kwa nini haukuwa na nidhamu binafsi na nguvu za uzingativu kidogo, ambazo zingekusaidia kupiga hatua mbele za mafanikio.
Jiulize, kitu gani, ambacho unaogopa kukifanya leo, ambacho miaka 10 ijayo pengine utakuja kujuta na kuanza kujilaumu, kwa nini sikufanya kitu hiki. Jiulize kitu hicho ni kipi?
Maisha ya thamani na mafanikio, yanajengwa sio kwa siku moja, bali yanajengwa kwa muda, siku hadi siku. Leo ni siku ambayo unatakiwa ujenge maisha hayo na fursa hiyo haiji mara mbili.
Kila siku ifanye iwe muhimu, ili kubadili maisha yako. Ukiifanya kila siku kuwa muhimu ya madiliko, miaka kumi ijayo, hutaweza tena kujishangaa, na kujiuliza maswali mengi.

0 Comments