BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Hamasa ya mafanikio ya leo.

Njia sahihi ya kulianza jambo, ni kuanza kulifanya na hakuna njia nyingine. Unatakiwa uanze kufanya na si kujiuliza wala kuogopa unatakiwa kuchukua hatua ya kuanza kufanya, basi.

Unapoanza kufanya, unapata uzoefu, ambao hauwezi kuupata kwenye vitabu au popote.  Kwa hiyo, hata uwe umesoma vitabu vingi vipi, kama hujaanza kufafanya hiyo ni sawa tu na bure.

Acha kusita sita, anza  kufanya. Hata kama ni kwa kujisukuma, kwa shida, mtaji hautoshi, unaona hatari, anza kufanya, kwani njia sahihi ya kuanza jambo lako ni kuanza kufanya.

Nguvu ya kufanikia ipo kwenye kuanza kufanya, hebu leo anza kufanya jambo lako na uone kama hautafika mbali kimafanikio. Ukianza kufanya, kaa ukijua utafanikiwa.


Post a Comment

0 Comments