BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Hamasa ya mafanikio ya leo.

Mafanikio ni kitu cha mtu binafsi, kile unachoona umefanikiwa wewe, kwa mwingine kinaweza kisiwe mafanikio. Kwa hiyo, Unatakiwa kuyapima mafanikio yako, kwa jicho lako, au kwa hatua zako, na si kwa jicho au hatua za mwingine.

Kwa mfano, unaweza ukajua vipi kama umefanikiwa au hujafanikiwa? Utajua kwa kuangalia mwendo. Unatakiwa uupime mwendo wako mwenyewe kila wiki, kila mwezi na ujue wapi ulipo na wapi unaenda na kipi kifanyike.

Mafanikio ni MCHEZO WA NAMBA, ili kufanikiwa unatakiwa ujue namba zako. Kwa mfano, unatakiwa ujue, kiasi gani cha pesa unacho benki? Wateja wangapi wa kudumu unao? Watu wangapi unawajua wa kukusaidia? Kama namba haziko sawa, unatakiwa kuzirekebisha.

Kumbuka, dunia haijali kitu gani kinakukuta wewe, unatakiwa kuchukua tahadhari wewe. Unatakiwa ujue wapi upo, na wapi unataka kwenda kimafanikio. Chukua jukumu la maisha yako kwa kupima mwendo wa mafanikio yako kibinafsi.


Post a Comment

0 Comments