BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Hamasa ya mafanikio ya leo.

Ipo ndoto ambayo unaiota na unataka kufika huko. Njia sahihi ya wewe kuweza kufikia mafanikio yako hayo unayoyataka, ni kuamua wewe mwenyewe kujisamehe kwenye baadhi ya mambo mambo.

Ninaposema kujisamehe, hapo yaani nikiwa na maana ni wewe kuamua kuacha baadhi ya mambo, hasa yale yanayokukwamisha kufanikiwa, huko ndiko kujisamehe ninakomaanisha haswaa.

Kwa mfano, kama unakata kuweka akiba, unatakiwa ujisamehe na matumizi ya hovyo ya pesa. Kama hutafanya hivyo akiba huwezi kuweka, na utajikuta kila siku akaunti yako inasoma sifuri, haina kitu.

Kama unataka kupunguza uzito, unatakiwa ujisamehe na kula vyakula vya mafuta futa, vyakula ambavyo havikusaidii. Inauma pengine kuacha kula nyama au chipsi lakini unalazimika kufanya hivyo ili uweze kufanikiwa.

Kama unataka kufanikiwa, unatakiwa ujisamehe na kuacha usingizi na starehe ambazo zitakutoa kwenye mstari wa kufikia mafanikio. Kila siku itabidi upige kazi haswa, usingizi na starehe zingine tupa hukoo.

Kwa hiyo, katika kila eneo unalotaka kufanikiwa, yapo mambo ya kuyasemehe ili malengo yako yatimie. Kama usipojisamehe na kuamua kuacha baadhi ya mambo,  huwezi kufanikiwa hata ufanyaje.


Post a Comment

0 Comments