BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Hamasa ya mafanikio ya leo.

 

Uadilifu ni kitu ambacho wengi wanakizungumza, lakini ni wachache ambao ni kweli ni waadilifu, wengi utakuta si watu waadilifu ubabaishaji mwingi sana umejaa.

Ni rahisi kuonyesha uadilifu, hasa pale mambo yanapoenda sawa, lakini mambo yanapoenda hovyo, hata wale ambao walikuwa ni waadilifu utashangaa uadilifu umewatoka.

Kama kweli unataka uwe mwadilifu wa kweli, unatakiwa uwe mwadilifu hata wakati ambapo mambo hayaendi sawa. Watu wenye mafanikio, ni waadilifu wakati wote.

Kuna mambo ya msingi ya kukusaidia, kama unataka kuwa mwadilifu kwenye maisha yako.

Moja, timiza ahadi unazozitoa. Kama kuna ahadi umezitoa zitekeleze moja kwa moja.

Mbili, ahidi kidogo na fanya makubwa ya uliyo ahidi. Ukifanya hivyo, utaheshimika sana.

Tatu, simamia maneno yako. Kile unachosema, ndio hicho uwe una maanisha na sio vinginevyo.

Nne, toa huduma yako, hadi unao wahudumia waridhike. Usiwaache watu walalamike huduma mbovu.

Tano, kuwa makini na kujua watu wanataka nini. Waelewe vizuri watu wanataka nini, kisha wape.

Sita, likitokea tatizo, litatue mara moja. Acha kuacha hadi tatizo liwe kubwa, tatua tatizo.

Unapokuwa mwadilifu inakusadia, kukuza mahusiano yako na wengine na hiyo itakusaidia kufika mbali kimafanikio. Ili uwe mwadilifu ndani yako, jitahidi sana, kujiheshimu na uwaheshimu wengine pia.


Post a Comment

0 Comments