Upo katika ulimwengu wa taarifa au habari, usipokuwa makini, utakuwa mtu wa kufatilia kila taarifa au habari na kujikuta ukisahau kufanya mambo yako.
Kitu cha kufanya unapokutana na habari nyingi, ili zisikuvuruge na ukashindwa kuchukua hatua, unatakiwa ufanye hivi;-
TUPA, kama taarifa au habari haihusiani na wewe na unaiona haikufai, itupe kule, huna haja ya kuifatilia, fatilia tena.
SAIDIWA, kama unaona habari au taarifa hiyo ni ya muhimu na huna muda wa kuifanya, omba mtu akusaidie kuifanya.
HATUA, ikiwa taarifa au habari unayoipokea ni muhimu kabisa, chukua hatua mara moja, usisubiri kesho au baadae, fanya.
HIFADHI, pia kama unaona taarifa au habari hiyo ni muhimu kwa baadae, iweke kwenye faili, utafanya siku nyingine ukitaka.
Hivi ndivyo, unavyoweza kushughulika, na ulimwengu wa taarifa au habari unaokuja kwako kwa kasi ya kimbunga.
(TUSAHAHI)

0 Comments