Jifunze kujua thamani ya muda wako na thamani ya maisha yako. Lazima, ujijue wewe ni wa thamani na una uwezo wa kutoa thamani kubwa kwa maisha yako na ya wengine pia.

Ili maisha yako yawe na thamani na uweze kutoa thamani inayotakiwa, inakubidi wewe ufanye mambo yafuatayo;-

a/. Jifunze kusema HAPANA.

b/. Weka NGUVU ZA UZINGATIVU eneo moja unalifanyia kazi.

c/. Acha kusimama KUJIFUNZA. Kila siku jifunze.

d/. Tatua MATATIZO mapema. Acha kuchelewa chelewa.

Hivi ndivyo unavyoweza kujua thamani ya maisha yako na maisha ya wengine pia.