BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Hamasa ya mafanikio ya leo.

 

Kufanikiwa kwako kwa kile unachokitaka, inakutaka sana wewe uzingatie mambo haya na kuchukua hatua za lazima.

a/ Decision/Maamuzi. Ni lazima uwe na maamuzi ya kwamba unataka kufanikiwa. Usipokuwa na maamuzi hayo ngumu kwako kwako kufanikiwa.

b/ Priorities/Vipaumbele. Hutafika popote kimafanikio kama huna vipaumbele, ni lazima wewe uweke vipambele vya kukusaidia  kukufanikisha.

c/ Descipline/Nidhamu. Nidhamu binafsi inahitajika sana kwa wewe kufanikiwa, bila hiyo utashindwa tu, maana utafanya mambo ya hovyo na utakwama.

d/ Commitment/Kujitoa. Ni lazima ujitoe ili kufanikiwa. Wanaofanikiwa ni watu ambao wanajitoa kufikia malengo yao. Hufanya linalowezekana ili kufikia mafanikio yao.

e/ 'Risk'./Kujitoa mhanga. Huwezi kufanikiwa kama hujiingizi kwenye mazingira hatarishi ya kukubali kupoteza pengine kila kitu. Elewa, kuna kupoteza unapotafuta.

f/ Effort/Juhudi. Ni lazima kuweka juhudi ili kufanikiwa . Wanaofanikiwa wanaweka juhudi siku hadi siku. Ni watu ambao hawachoki kuweka juhudi hizo.

g/ Focus/Nguvu za uzingativu.  Akili yako lazima itulie ili uweze kufanikiwa. Weka akili yako katika sehemu moja tu. Acha kuyumba yumba, utapotea.

h/ Stregth/Uimara.  Ili kufanikiwa lazima uwe imara. Unatakiwa usiwe mwepesi sana kuyumba yumba. Ukiwa imara utafanikiwa, kinyume cha hapo utashindwa.

Usiogope kushindwa, kwani kushindwa ni njia mojawapo ya wewe kuyafikia mafanikio yako. Ukizingatia mambo hayo utapiga hatua za mafanikio.


Post a Comment

0 Comments