BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Hamasa ya mafanikio ya leo.

 

Ni rahisi sana kufanya mambo ambayo watu wengine wanategemea ufanye. Watu wengine wana viwango vyao ambavyo wamekuwekea wewe ufike kimafanikio. Ni watu ambao hawaamini kama unaweza kufika mbali na hapo.

Kwa sasa angalia kufanya zaidi ya kile kinachotegemewa. Tayari unafanya kile kinachotegemewa. Kwa kuongeza juhudi kidogo, basi utafanya makubwa zaidi ya yale yanayotegemewa. Juhudi za ziada ndio kila kitu katika kuweza kukufanikisha.

Kwa kuongeza juhudi kidogo, kwa kwenda hatua kidogo za ziada, hiyo itakusaidia kwenda mbali kimaisha na kufanya makubwa tofauti na ilivyo tegemewa na wengi.  Mambo makubwa utayapata kwa wewe kwenda hatua za ziada.

Haitumii nguvu nyingi sana, kutoka kwenye maisha ya watu wa kawaida, hadi kwenda kwenye maisha ya watu ambao wamefanikiwa. Kinachotakiwa ni kwa wewe kufanya kama unavyofanya kila siku, ila ongeza juhudi kidogo tu, UTAFANIKIWA.


Post a Comment

0 Comments