BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Hamasa ya mafanikio ya leo.

 

Inataka ujasiri na kujiamini sana, kuweza kuishi maisha ya ndoto zako. Pasipo ujasiri na kujiamini huwezi kuishi maisha hayo. Kuna wakati akili inatuambia basi imetosha, lakini wewe hutakiwi kuishia hapo na kurudi nyuma,  unatakiwa kwenda mbele na moyo wa ujasiri na kujiamini hata kama akili imegoma.

Ujasiri na kujiamini kwako,  utaendelea kuja kwa jinsi unavyoendelea kuchukua hatua, kwa jinsi unavyokutana na changamoto na kwa jinsi unavyokabiliana na hofu.  Inataka ujasiri na kujiamini, kuishi maisha ya ndoto zako.

Kila kitu kitakaa sawa, na utaweza kufikia ndoto zako, ikiwa utakuwa na ujasiri na kujiamini.  Wewe kazana tu, kutengeneza ujasiri na kujiamini kwako, na maisha yako yatajitengeneza hivyo hivyo. Hutaweza kushindwa, ikiwa utakuwa jasiri na kujiamini.


Post a Comment

0 Comments