Kila wazo unalowaza, linajenga maisha yako au tabia yako, pasipo kujali maisha hayo ni mazuri au mabaya. Hiyo iko hivyo ni kama vile matofali yanayojenga nyumba yanavyokuwa, na mawazo yako yanajenga maisha yako hatua kwa hatua na siku hadi siku.
Kwa jinsi utakavyokuwa kesho, au kwa jinsi maisha yako yatakavyokuwa kwa kesho, inategemea sana mawazo unayoyajenga kila siku ni ya aina gani. Ni wazi kama una mawazo mazuri basi unakuwa unajenga maisha yako mazuri, lakini kama una mawazo mabaya na maisha yanakuwa ya hovyo.
Kila wazo ulilonalo, na kila wakati, kaa ukijua linatumika kukujenga wewe. Ndio maana hakuna mafanikio yanayoweza kutokea kimuujiza, mafanikio yanajengwa tena kupitia mawazo yako. Unaweza kujenga maisha unayotaka, kikubwa tumia mawazo yako vizuri.
Mpaka sasa unajenga maisha yako, kupitia maamuzi unayoyachukua, na pia hatua unazochukua. Hii ni nafasi ya dhahabu uliyonayo ya kubadili maisha yako na kuyafanya kuwa bora kabisa kupitia mawazo yako. Kila wakati chagua kuwa na mawazo bora ya kukujenga na utafanikiwa sana.

0 Comments