BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Hamasa ya mafanikio ya leo.

Wale wanaofikia mafanikio, ni watu ambao wanayaona mafanikio na kuchukua hatua kutokana na jinsi wanavyoyaona mafanikio hayo.

Kuna mafanikio katika eneo la baridi sana kwa watu wanaona ipo haja ya kuuza makoti na kutoa vifaa vya kutolea joto, mafanikio hayo yapo.

Kuna mafanikio katika mafuriko, na mafanikio yapo kwa watu wanaona kwamba wanaweza, wakajenga nyumba za watu waliothirika.

Kuna mafanikio katika jangwa, kwa watu wanaona wanaweza kuwapelekea chakula na maji hasa kwa watu wanaoishi jangwani tena kwa tabu.

Pia kuna mafanikio kwenye shida za usafiri, kwa watu wanaona kwao ni rahisi kununua magari na kuwapa watu hao ambao wana shida za usafiri.

Mafanikio yapo kila sehemu ikiwa utayaona mafanikio hayo. Katika kila hali, ipo MBEGU YA MAFANIKIO YAKO, hata kama hali hiyo unaiona ni mbaya. Watu wenye mafanikio hawasubiri hadi hali ziwe bora na hawalaumu kitu, bali wanachukua hatua.

Kufikia mafanikio makubwa kunakuja kwako kwa wewe kuamua kuyaona mafanikio, na kuamua kujitoa, kuweka juhudi, nidhamu na nguvu zako zote za uzingativu hapo. Tafuta mafanikio yako popote ulipo, kama utayaona, kwa jicho la ndani, basi umefanikiwa.


Post a Comment

0 Comments