BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Hamasa ya mafanikio ya leo.

Hakuna tofauti kubwa sana na ya wazi kwa wale wanaoshinda mbio na wale ambao huwa wanashindwa. Tofauti hiyo kubwa haipo, kwa maana wote hao wana kila kila kitu karibu kilicho sawa, ikiwa pamoja na vifaa vya mazoezi sawa, sheria zile zile,  misuli iko sawa na vitu vingi tu viko sawa.

Hata ukiangalia mtu yule mwenye wateja wengi sana, na yule ambaye ana wateja wa kawaida, wote wawili wana ujuzi na rasilimali sawa. Tofauti inakuja, ni nini wanafanya kwa kile walichonacho.

Mtunzi wa riwaya anayeuza zaidi, na mwandishi ambaye hajachapisha vitabu, wote wana kamusi sawa iliyojaa maneno ya kufanya kazi nayo. Tofauti kubwa inakuja ni nini wanafanya kwa kile walichonacho.

Lakini kinachofanya washindi katika mbio kuweza kushinda, ni ule moyo wa kuweza kujitoa kushinda. Washindi wanakuwa wanaoongoza juhudi kidogo tu na kushinda. Kila siku washindi wanakuwa wanakwenda hatua za ziada za kuwafanikisha.

Unatakiwa uelewe, tayari una rasilimali za kukuwezesha kufanikiwa. Tayari una kile kinachohitajika ili kufanikiwa. Ndani yako una uwezo wa kufikia mafanikio yoyote, unachotakiwa kufanya ni WEWE KUAMUA KWENDA HATUA ZA ZIADA TU.


Post a Comment

0 Comments