Ikiwa unafanya kitu halafu ukaishia kati, au ukaacha huku ukiwa umefikia asilimia 99% basi kaa ukijua ndio utakuwa umeshindwa, na unakuwa sawa na mtu ambae hajaanza tu, yaani wote mnakuwa mmeshindwa.
'Pointi' ya msingi kuizingatia ni kwa wewe kwenda mbele kwa chochote unachokifanya, na hutakiwa kuishia kati, unatakiwa ufike mwisho, maana ushindi haupatikani kwa wewe kuishia kati, unatakiwa ushinde.
Tambua vizuri kile unachokifanya, na endelea kukifanya hadi uweze kufanikiwa. Acha mchezo wa kuishia kati, maana ukiishia kati hutaweza kufanikiwa, sana sana utashindwa vibaya na utakuwa umepotea kabisa.

0 Comments