Huwezi kuwa imara katika mambo makubwa, kama uimara huo hauna hata kwenye mambo madogo. Uimara wa wewe katika mambo makubwa, unajengwa na uimara wewe katika mambo madogo madogo tu.
Kwa mfano, huwezi kuwa biashara ndogo, kama hujawahi kuwa hata mfanyabiashara mdogo. Pia kama wewe ni mnyanyua vyuma, huwezi kubeba vyuma vizito, ikiwa hujawahi kubeba vyuma vidogo.
Mpaka hapo unaona uimara wako, unajengwa kwanza na mambo madogo. Mafanikio yako yanataka uwe imara. Na uimara huo hauji kizembe tu, unakuja kwa wewe kuwa hodari wa kufanya mambo madogo kwanza.
Kuwa tayari, kuwa hodari sana kwa kufanya mambo madogo, na mambo hayo madogo, yatakusaidia kuwa imara na kufikia mafanikio makubwa.

0 Comments