BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Hamasa ya mafanikio ya leo.

Chochote kila unachokitaka ni lazima ukilipie gharama. Huwezi kupata unachokitaka bila ya kulipia gharama na huo utakuwa ni uongo, gharama ni muhimu kuzilipia. Na zinaweza kuwa gharama za pesa au sio pesa.

Kwa mfano, kama unataka kuwa mfanyabiashara mkubwa, lazima ulipie gharama za ubunifu, kujitoa, kufanya kwa nguvu na hata kuingia kwenye 'risk', hizo ndo gharama baadhi unatakiwa kuzijua na kuingia.

Na ili uweze kuwa na maisha bora, ni lazima uweze kuingia kwenye gharama ya wewe kuweka juhudi, kujitoa, nidhamu binafsi na kuweka nguvu za uzingativu, hizi ni gharama za lazima ili kuwa na maisha bora.

Hata hivyo unatakiwa kujua, chochote unachokitaka, ni lazima uweze kuingia gharama ili kukipata. Leo hii, jua kile unachokitaka na kisha amua kuingia gharama ili kukipata kitu hicho, vinginevyo hutaweza kukipata.


Post a Comment

0 Comments