Katika safari ya kufikia mafanikio yetu, mara nyingi zipo changamoto za kweli, yaani changamoto za nje, na zipo changamoto ambazo si za kweli bali ni changamoto zinazotokana na mawazo yetu wenyewe.

Kuna wakati mawazo yetu, yanatuambia, huwezi kufanya hiki, au pia yanatuambia jambo hili ni hatari, liogope na achana nalo. Hizi ni changamoto zinatokana na mawazo na huwa si za kweli mara nyingi.

Kikubwa kwako, unatakiwa kuangalia, kama ni changamoto unakutana nayo, je, ni ya kweli au inatokana na mawazo yako tu. Kama ni changamoto inayotokana na mawazo yako chunguza mawazo yako hayo mara mbilimbili.

Kumbuka, changamoto zipo za aina mbili, changamoto za kweli, zinazotokana na mazingira halisi, na changamoto za mawazo yetu, je, wewe changamoto zinazokuzuia kufanikiwa ni zipi? Tatua changamoto hiyo na ufanikiwe.