BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Hamasa ya mafanikio ya leo.

 


Inawezekana unaogopa kuchukua hatua, kwa sababu hauna uhakika na maamuzi unayoyafanya, kama ni maamuzi sahihi au sio maamuzi sahihi kwako. Na unaogopa sana na kujiuliza, je, ikiwa sio maamuzi sahihi, itakuwaje?

Watu wenye mafanikio kikubwa wanachoangalia ni kule kuchukua hatua, na si kuangalia sana juu ya maamuzi yao kama ni sahihi au sio sahihi. Hata wakikosea huwa wanajipa nafasi ya  kujirekebisha na kusonga mbele.

Unatakiwa uelewe, hata uwe mtaalamu vipi, huwezi kufanya maamuzi sahihi kila wakati. Kaa ukijua kuna kukosea katika kufanya maamuzi yako, hivyo usiwe mhanga wa kutaka kufanya maamuzi sahihi tu kila wakati.

Ili kufanikiwa, acha kuganda kwenye kutaka kuwa na maamuzi sahihi, na ukasahau kuchukua  hatua. Lakini pia, usikosee kwa makusudi, fanya maamuzi yako sahihi, ukikosea, utajirekebisha na hakuna kujuta wala kulia.


Post a Comment

0 Comments