BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Hamasa ya mafanikio ya leo.

 

Muda sahihi zaidi wa mashua kusafiri na upepo,  ni wakati mashua inaelekea  karibu kukutana na upepo huo. Vivyo hivyo, njia ya haraka ya wewe kufanikiwa ni  kukutana na vizuizi au changamoto za  moja kwa moja.

Ni kupoteza muda, juhudi na nguvu zako bure, kwa kuendelea kukimbia na kuzunguka changamoto, zinazokuzuia kufanikiwa. Ni bora kukutana na changomoto hizo moja kwa moja, kisha uzitatue na uendee mafanikio yako.

Kwa mtazamo sahihi ulionao, changamoto unazokabiliana nazo zitakusaidia kukupa nguvu na hamasa ya kuwa mshindi. Kama mashua inayosafiri kwa upepo inahitaji nguvu, umakini na kujitoa. Hata wewe unahitaji vitu hivyo ili kufanikiwa.


Post a Comment

0 Comments