Ikiwa umefanikiwa kuyafikia malengo yapo, hapo ndipo unatakiwa uwe makini sana. Kama usipokuwa makini, kaa ukijua kuna changamoto, ambazo zinaweza zikakushusha toka kilele hicho cha mafanikio.
Sio kwa sababu wewe ni mshindi, hiyo ikiwa na maana kwako utabaki hapo milele au hutaweza kushuka tena, haipo hivyo. Unatakiwa kuwajibika na kuwa makini na changamoto za kukaa juu ya kilele cha mafanikio.
Hakuna kituo kimoja cha ushindi. Ukiona leo ni mshindi kwenye jambo moja, jiandae kushinda katika jambo lingine pia. Usipojiandaa, hata lile jambo uliloshinda utakwama tena. Kuwa mshindi, lakini jiandae na changamoto zake.

0 Comments