Pengine unajiuliza sana, ni siri au ipi kanuni ipi hasa ya mafanikio ambayo kila mtu akiitumia ni lazima atafanikiwa? INATEGEMEA, nikiwa na maana hakuna kanuni ya moja kwa moja ya mafanikio ambayo kila mtu akiitumia lazima afanikiwe.
Kanuni hiyo haipo kwa sababu inategemea maarifa uliyonayo, watu unaowajua, kipi unakitaka na kipi unakifanya. Hakuna jibu la moja kwa moja, kwamba hii ndio njia sahihi ya mafanikio yako, jibu hilo kaa ukijua halipo kabisa.
Hakuna mtu atakayekwambia ya kwamba njia sahihi ya mafanikio ni hii au jibu sahihi la mafanikio yako ni hili, yote inategemea. Ni wajibu wako wewe kuchukua hatua na kuwajibika kulingana na unavyoona mwelekeo wako upi ni sahihi kukufanikisha.
Amua leo kuchukua jukumu la maisha yako kwa asilimia mia, na utaona ndoto zako unaanza kuzifikia na kubadili maisha.

0 Comments