Mara nyingi vitu unavyovithamini, ndio vinakuwa vitu vya thamani sana katika maisha yako. Siku zote, thamani ya kitu inatengenezwa kwa umakini wako, juhudi zako na kujitoa kwako.
Kwa mfano, ipe thamini kazi yako na kazi hiyo itakuwa ya thamani zaidi. Ipe thamani nyumba yako na nyumba hiyo itakuwa ya thamani zaidi. Thamini maisha yako, familia yako, imani yako, mwili wako, pesa, muda na akili yako - na vyote hivyo vitakuwa vya thamani zaidi kwako.
Mpaka hapo unaona chochote kile unachokithamini, lazima kiwe na thamani tu. Na thamani ya kitu haipo kwenye bei tu. Thamani ya kitu chochote ni thamani unayoipa. Hakikisha, unajitoa haswa kwa vitu ambavyo unavithamini na hakika vitastawi na kuwa vyako.

0 Comments