BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Hamasa ya mafanikio ya leo.

Miti mikubwa na hodari ina tabia moja kubwa, kabla haijakua kwenda juu angani, huanza kwanza kupeleka mizizi chini na kwa umbali mrefu, ili kusaidia kutafuta maji na chakula kitakachoifanya ikue na iwe mirefu sana.

Kwa kila mti ambao unakua sana kwenda juu, kwa kawaida huwa ni mti ambao tayari una mizizi mirefu sana na ambayo huwezi kuiona, lakini mizizi hiyo inakuwa imezama ndani zaidi kwa chini ili kusaidia ukuaji wa mti huo kwenda juu zaidi.

Tunapowaangalia watu waliofanikiwa, mara nyingi tunaona mti, lakini sio mizizi. Mafanikio yao tunakuwa tunayaona rahisi sana kwa sababu tunashindwa kuona bidii, kujitoa, nidhamu na maandalizi yote ambayo yalikwenda kuweka msingi - mizizi - ya mafanikio yao.

Mafanikio ya kudumu yanawezekana tu kama umejenga msingi thabiti wa nidhamu na maandalizi bora kama ilivyo mizizi ya miti inayokwenda chini sana.


Post a Comment

0 Comments