BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Hamasa ya mafanikio ya leo.

Tishio kubwa la kujifunza lipo kwa wewe kukataa kujifunza zaidi. Hiyo iko hivyo yaani kadri, unavyojifunza unaona haina haja ya kujifunza tena kwamba uliyojifunza yametosha.

Kama unaona umetosheka mara baada ya kujifunza, nikwambie ndio utakwama sana na utaanza kurudi nyuma. Kushindwa kunaanzia pale unapokataa wewe mwenyewe kujifunza.

Kama kweli umeamua kupiga hatua, amua kujifunza iwe ndo silaha kubwa ya kukufikisha kwenye mafanikio hayo makubwa. Jifunze kwenye vitabu au semina na utafanikiwa.

Kila siku jifunze, kua, na chukua hatua. Ikiwa ndio mwendo utakuwa huo utafika mbali sana baada ya muda si mrefu, maana ukijifunza na kuchukua hatua, ni lazima utapiga hatua.


Post a Comment

0 Comments