BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Hamasa ya mafanikio ya leo.

 

Moja ya kitu hatari cha kuweza kukitawala, ni kisu chenye makali sehemu mbili. Kisu hicho ni hatari kwa sababu matumizi yake yanataka umakini mkubwa na wakati wowote kinaweza kikakukata.

Kama unavyoona matumizi ya kisu chenye makali pande mbili yanataka umakini wa hali ya juu, hata wewe mawazo yako na matendo yako, vinataka umakini mkubwa sana kwako, ili visije vikakudhuru.

Mawazo uliyonayo na hatua unazochukua kidogo kidogo kila siku, vitu hivi vina matokeo kila siku katika dunia yako, hata kama matokeo huyaoni leo, lakini yataonekana tu kwa baadae.

Hivyo, unatakiwa kuwa makini sana na mawazo yako na vitendo vyako, maana ni kama kisu chenye makali sehemu mbili. Ukitumia vizuri mawazo na matendo yako utafanikiwa na ukitumia vibaya utashindwa vibaya sana.


Post a Comment

0 Comments