Maisha yako yatakuwa bora sana, kama utaamua kuacha kusubiri mambo yatokee yenyewe na kufanya mambo yatokee. Badala ya kulaumu wengine, fanya kitu, badala ya kusema kwa nini hili limetokea kwangu, jiulize nitafanya nini juu ya hili.
Unatakiwa uweke mipango yako imara ya kufikia malengo yako. Hakuna kitu au kizuizi ambacho kinaweza kukuzuia kufanikiwa ikiwa kweli utakuwa una dhamira ya kufikia malengo yako.
Nguvu yako kubwa ya mwelekeo, kujitoa, na hatua unazochukua hizo ndizo zitakazofanya mambo yako yatokee na si kusubiri hadi yaweze kutokea yenyewe kama muujiza. Kuendelea kusubiri mambo yatokee yenyewe ni kujichelewesha huko.
Ili kufanya mambo yatokee, unatakiwa kila wakati kuwajibika kwenye mawazo yako, maneno yako, imani yako na vitendo vyako. Ukiweza kuwajibika katika maeneo hayo, basi utafanya mambo kutokea.

0 Comments