Kitu chochote ambacho kweli una kimiliki, ni kitu ambacho unaweza kukitoa kwa wengine. Kama huna uwezo wa kutoa kitu hicho kwa wengine, basi bado wewe si mmliki wa kitu hicho bali ni mtumwa wa kitu hicho.
Utakuwa kweli una maarifa sahihi, upendo wa dhati, furaha ya kweli na pesa za halali na zako, kama kweli vitu hivyo unavitoa pia kwa wengine bila choyo. Kama vitu hivyo unavitoa kwa wengine, basi ni kweli unavimiliki.
Kwa chochote kile ambacho unacho na unaweza kutoa kwa wengine, basi kweli kitu hicho una kimiliki kweli. Haimaanishi utoe vitu vyote ulivyonavyo, hapana. Kile unachotoa kiwe ziada kwa sababu unacho.
Utajiri wa kweli kwako unapatikana kwa wewe kutumia vile ulivyonavyo iwe kwako na kwa wengine pia.

0 Comments