Haijalishi ni matatizo gani unayopitia, haijalishi ni changamoto zipi kubwa unazopitia. Hayo yote bado ni madogo sana, ukilinganisha na wingi wa utajiri mkubwa ambao dunia hii inao.
Kwa bahati nzuri unaishi. Na tena unaishi kwenye dunia yenye fursa za kutosha. Una uwezo wa kufanya makubwa unayotaka. Una uwezo wa kufanya mabadiliko yoyote kwenye maisha yako, kwa sababu maarifa ya kufanya hivyo yapo.
Unatakiwa ujue, matatizo na changamoto unazopitia sasa, ni za muda tu na pia sio sababu ya kukuzuia kufanikiwa. Dunia uliyopo imejaa mafaniko, huhitaji kujuta wala kulia. Ni uamuzi wako kufanya utakalo.
Ni jukumu lako, kutumia wingi wa fursa kufanikiwa na acha kuumizwa sana na changamoto unazopitia leo ambazo pia ni za muda tu na zitaisha.

0 Comments